Huwezi kusikiliza tena

Ethiopia tayari kwa uchaguzi jumapili

Muungano wa Afrika umesema Ethiopia iko tayari kwa uchaguzi mkuu wa jumapili. Kiongozi wa timu ya waangalizi wa AU ifikepunye Pohamba anasema kampeni na maandalizi ya uchaguzi huo zimekuwa za amani. Hata hivyo ameitaka Ethiopia kuangalia upya sheria kadhaa kuhusu vyombo bya habari na za kukabiliana na ugaidi ambazo anasema huenda katika siku za usoni zikahujumu uhuru wa raia wake kushiriki katika uchaguzi. Pohamba ambaye ni rais wa zamani wa Namibia, amesema timu yake ya wachunguzi zaidi ya sitini wameridhishwa na maandalizi ya uchaguzi huo wa Mei 24. Zaidi ya raia milioni thelathini na sita wamejisajili kushiriki uchaguzi huo. Mwandishi wetu Emmanuel Igunza na mengi zaidi kutoka mji mkuu wa Addis Ababa...