Huwezi kusikiliza tena

Mfahamu msichana anayedaiwa kwenda Syria

Siku chache tu baada ya kuibuka kwa taarifa nchini Kenya, kwamba Salwa Amir, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta mjini nairobi - amesafiri hadi Syria, hii ikiwa ni baada ya familia yake kuripoti kwamba amepotea, wengi wametaka kujua zaidi kumhusu na jinsi chuo hicho kilivyohisi baada ya kupokea taarifa hizo.

Mwandishi wetu Abdinoor Aden ametembelea chuo hicho na kuzungumza na Abdalla kheir, mhadhiri katika chuo hicho na mkuu wa wanafunzi wa kiislamu.