Huwezi kusikiliza tena

Jamil Mukulu kupelekwa Uganda?

Kiongozi wa kundi la waasi wa ADF kutoka Uganda, Jamil Mukulu, leo anatarajiwa kufika mahakamani nchini Tanzania kusikia endapo pingamizi lake la kutaka asirejeshwe Uganda kukabiliwa na mashataka mbali mbali limekubaliwa au la. Kiongozi huyo aliyekuwa mafichoni kwa miaka mingi, alikamatwa na polisi wa Tanzania mwezi uliopita kutokana na maombi ya Uganda kupitia polisi wa kimataifa Interpol.Wiki iliyopita mahakama ilimpa Mukulu muda wa kuwasilisha pingamizi kabla ya uamuzi kutolewa endapo arejeshwe Uganda ambako anakabiliwa na mashtaka mazito ikiwemo mauaji.Hassan Mhelela ana maelezo kutoka Dar es Salaam.