Polisi afutwa kazi kwa kudhulumu weusi
Huwezi kusikiliza tena

Polisi afutwa kazi kwa kudhulumu weusi

Polisi mmoja mzungu katika jimbo la Texas nchini Marekani amesimishwa kazi baada ya video moja kuwekwa kwenye mitandao ikionyesha akihangaisha kundi moja la vijana wengi wao wakiwa ni weusi.

Afisa hiyo anaonekana akiwalenga vijana wawili wa kiume kwa bunduki yake huku pia akimuangusha chini na kumkamata msichana wa umri wa miaka 14.

Polisi hao walikuwa wameitwa na wenyeji waliokuwa wakilalamikia kuwepo usumbufu kwenye kidimbwi kimoja cha kuogelea.