Dr Simon Lokodo,waziri wa maadili nchini Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Ngono badala ya chakula nchini Uganda

Baadhi ya wananchi wa Uganda wametoa maoni tofauti kufuatia kauli iliyotolewa Waziri anayehusika na maadili nchini humo Dokta Simon Lokodo.

Dokta Lokodo ameripotiwa akisema kwamba kiwango cha maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi kimekuwa kikubwa kutokana na kile alichokieleza kwamba hivi sasa watu wanachagua kufanya ngono badala ya kwenda kula chakula cha mchana.

Aliyasema hayo mjini Gulu na kusisitiza kuwa tendo la ndoa kwa sasa, limekosa maana hasa kwa vijana.

Halima Nyanza amezungumza na Mwandishi wa BBC mjini Kampala Siraj Kalyango, kutaka kujua kauli hiyo ilivypokelewa.