Nepal kufungua upya vivutio vya watalii
Huwezi kusikiliza tena

Nepal kufungua upya vivutio vya watalii

Serikali ya Nepal imetangaza kuwa itafungua upya vivutio vya watalii vilivyoharibiwa na tetemeko la ardhi.

Hatua hiyo ya serikali ya kuwavutia watalii hata hivyo imetiliwa shaka na UNESCO ambayo inahofia kuwa huenda maisha ya watalii yakawa hatarini.

Serikali ya Nepal imekuwa mbioni kunadi vivutio vyake huku ikiharakisha shughuli ya ukarabati wa vituo vilivyoharibiwa katika tetemeko hilo