Wazazi wa mwanaharakati mmoja wa haki za raia nchini Marekani wamesema kuwa anajifanya kuwa mtu mweusi kwa miaka kadhaa sasa
Huwezi kusikiliza tena

Mwanaharakati anayejidai kuwa ''Mweusi''

Wazazi wa mwanaharakati mmoja wa haki za raia nchini Marekani wamesema kuwa anajifanya kuwa mtu mweusi kwa miaka kadhaa sasa.

Rachel Dolezal analifanyia kazi shirika liitwalo National Association for the Advancement of Colored People {NAACP} huko Spokane takriban maili 280 mwa mji wa Seattle kazkazini magharibi mwa Marekani.

Kulingana na msemaji wa gazeti la Review,Dolezal amesema kuwa yeye ni mchanganyiko wa mtu mweupe,mweusi na muhindi wa Marekani katika ombi lake alilowasilisha kwa tume ya polisi inayosimamia malalamishi ya raia mnamo mwezi Januari.