Kundi la Taleban lashambulia bunge Afghanistan
Huwezi kusikiliza tena

Taleban yashambulia bunge la Afghanistan

Serikali ya Afghanistan inasema kuwa imefanikiwa kusitisha shambulio katika bunge na kuweza kuwaua washambuliaji wote.

Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo lilianza na kulipuka kwa gari lililotegwa vilipuzi nje ya bunge kabla ya ufyatuzi wa roketi na risasi.