Bunge la Kenya likiendelea na vikao vyake
Huwezi kusikiliza tena

Muswada tata wapendekezwa Kenya

Nchini Kenya, mswada wa kutatanisha unaopendekeza vijana walio na umri wa chini ya miaka 20 kupewa vidonge vya kuzuia mimba bila idhini ya wazazi umefikishwa kwenye bunge la senate. Mswada huo pia unapendekeza kutolewa kwa mafunzo ya uzazi katika shule nchini humo ili kuepusha jamii kutokana na kile kinachotajwa kama mimba za mapema miongoni mwa wasichana. Swali ni je, kuna haja ya mzazi kutoa idhini mwanawe kupata huduma za mpango wa uzazi wa kisasa? Sikiliza maoni ya baadhi ya wakaazi wa Dar es salam kuhusu mswada huu.