Francois Hollande
Huwezi kusikiliza tena

Hollande achunguzwa na NSA ?

Mtandao wa Wikileaks umechapisha nyaraka zinazoonyesha kuwa chombo cha upelelezi cha Marekani NSA kimemchunguza rais wa Ufaransa, Francois Hollande, na marais wawili waliokuwa kabla yake.

Inaaminika kwamba upelelezi huo umefanyika kati ya mwaka 2006 na 2012. Idara ya Marekani haikuweza kuthibitisha usahihi wa nyaraka hizo.

Mwandishi wa BBC aliyopo mjini Washington amesema kuwa upelelezi uliofanywa kwa viongozi wa Ujerumani, Brazil na Mexico ndio wa hivi karibuni zaidi kufanyika.Moja wapo ya mazungumzo ya simu yaliyochunguzwa ni yale yanayomwonyesha rais Hollande akiidhinisha kufanyika kwa mikutano ya siri mapema hapo mnano mwaka 2012 kuhusu madhara ya kujitoa kwa Ugiriki katika Umoja wa Ulaya.

James Woolsey amewahi kuwa mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA.Amesema kwa nchi kuchunguza washirika wake ni jambo linalokea sana na hasa linahusishwa na masuala ya kiuchumi:

"sitapenda kumtuhumu mtu yeyote kuhusiana na Ufaransa lakini kuna baadhi ya nchi ambazo zinatumia taarifa zao za kiintelijensia kuchunguza kuhusu utuaji wa mikataba kimataifa ili kusaidia mashirika ya nchi zao, kusaidia hayo mashirika kutoa hongo kwa wengine ili mashirika ya nchi zao yapewe mikataba. Watakaposita kutoa hongo, basi na sisi tutaacha kuchunguzana."

Omar Mkambala ametuandalia taarifa ifuatayo: