Huwezi kusikiliza tena

Umewahi kula konokono?

Mfanyabiashara mmoja nchini Kenya ameanzisha kampeni kali ya kufuga konokono Afrika Mashariki. Konokono huliwa kwa wingi maeneo ya Afrika Magharibi lakini wenyeji wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika hawajakuwa na tabia ya kula konokono. Wataalamu wanasema kuwa ufugaji wa konokono ni kilimo nafuu chenye faida kubwa. Mwandishi wetu Ruth Nesoba amekuwa katika eneo la pekee kunakofugwa konokono Afrika mashariki na kutuandalia taarifa ifuatayo.