Kenya yawateua mabondia 10 kushiriki katika michuano ya Afrika
Huwezi kusikiliza tena

Kenya yawateua mabondia wa ndondi za Afrika

Chama cha ndondi cha Kenya kimechagua mabondia 10 wanaume na watatu wa kike watakaoshiriki michezo ya mataifa ya Afrika nchini Congo Brazaville mwezi Septemba mwaka huu. Mabondia hao walichaguliwa baada ya mashindano ya siku tatu katika ukumbi wa Kaloleni jijini Nairobi....John Nene alikuwa kando ya ulingo jana katika fainali ya mashindano hayo, na hii hapa ripoti yake.