Mtoto aliyezaliwa
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yapunguza vifo vya watoto

Wakati tarehe ya mwisho ya tathmini ya malengo ya maendeleo ya milenia ikikaribia , nchi ya Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo zimefanikiwa kutimiza lengo namba nne linalolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa theluthi mbili. Pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya watu, nchi hiyo imeweza kupunguza asilimia 39 ya vifo vya watoto. Bila shaka hii ni habari njema lakini bado mapambano yanaendelea kama anavyotuarifu mwandishi wetu Tulanana Bohela