Duka la West gate kufunguliwa
Huwezi kusikiliza tena

Duka la West Gate kufunguliwa

Jumba la Westgate jijini Nairobi nchini Kenya lililoshambuliwa na magaidi wa Alshabab miaka miwili iliyopita linatarajiwa kufunguliwa upya mwishoni mwa wiki hii. Wakati wa mashambulizi hayo ya mwezi Septemba mwaka 2013 watu Wasiopungua 67 waliuawa. Tayari ukarabati umefanywa katika jengo hilo huku wawekezaji katika maduka ya kifahari wakianza kuweka bidhaa tayari kwa mauzo. Mwandishi wa BBC Abdi Noor Aden amekwenda kuzuru jumba hilo na kutuletea taarifa ifuatayo.