Huwezi kusikiliza tena

Wanajeshi wauawa Marekani

Mtu mwenye silaha amewaua askari 4 wa jeshi la wanamaji wa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo ya jeshi hilo.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja kwenye mji wa Chattanooga, Tennessee.

Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

Sikiliza mahojiano kati ya Halima Nyanza wa BBC na Profesa Fulbert Namwamba mkazi wa Marekani, kwanza kuhusiana na mauaji hayo yaliyopokelewa Marekani kwenyewe.