Diamond na khadija kopa
Huwezi kusikiliza tena

Khadija Kopa awatumbuiza mashabiki Uingereza

Wakati tunasherehekea Eid Ul Fitri kote duniani, kwa wale waliosherehekea siku ya Ijumaa na wale waliosherehekea siku ya jumamosi, mbwembwe na shangwe ni zile zile, Malkia wa Twaarab Afrika Mashariki na Kati Khadija Kopa yuko Uingereza kuwatumbuiza mashabiki wa Modern twaarab wakati wa sherehe hizi za Eid, ametutembelea studio zetu hapa jijini London na mwenzangu Mariam Omar amezungumza naye, kwanza amemuuliza hii kolabo mpya amefanya na msanii wa bongo Flava Diamond ina maana anahamia katika maeneo hayo?