Mama Sarah Obama asema rais Obama atazuru Kogelo kumtembelea
Huwezi kusikiliza tena

Ana kwa ana na bi Sarah Obama

Huku Wakenya wanaposubiri kwa hamu kuwasili kwa Rais wa Marekani, Barack Obama, mnamo Ijumaa, jijini Nairobi ili kufungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kuna wengi wanaojiuliza iwapo atatembelea nyumbani alikozaliwa baba yake katika kijiji cha Kogelo, Magharibi mwa Kenya. Muliro Telewa alimtembelea bibi yake, Mama Sarah Obama kujua anavyojiandaa kumkaribisha mjukuu wake maarufu Barack Obama.