Urembo katika visiwa vya Comoro
Huwezi kusikiliza tena

Urembo katika visiwa vya Comoro

Bila shaka urembo unaweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali.

Na nchi tofauti zina namna ya kipekee kudhihirisha uzuri wao.

Zuhura Yunus alikuwa katika visiwa viwili miongoni mwa vinne vinavyounda Comoro, (Nzwani na Mayotte), na akiwa mtaani alikutana na wanawake waliokuwa wamejipaka kama podari nyeupe iliyoganda usoni.

Afrika Mashariki hasa maeneo ya pwani huita Liwa, ambapo aghlabu wanawake hupaka wakiwa ndani na husafisha uso wakitoka nje.

Hata hivyo visiwani humo mambo ni tofauti, msinzano kama wanavyouita unaelezwa zaidi na mkazi wa Nzwani Hasanati Suleiman.