Huwezi kusikiliza tena

Yemen bado si shwari

Muda mfupi baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, kumezuka mapigano kusini mwa Yemen.

Mashuhuda wanasema waasi wa Houthi wameshambulia maeneo ya raia karibu na mji wa Taiz. Lakini mji mkuu Sanaa na katikati mwa nchi hiyo umeelezwa kuwa shwari. Sikiliza mahojiano ya Halima Nyanza na Mchambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati, Ahmed Rajab, ambaye kwanza anaelezea juu ya maana ya usitishwaji mapigano.