Machimbo yazua maafa nchini Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Machimbo yazua maafa Kenya

Wasiwasi unaibuka miongoni mwa wakazi wa pwani ya Kenya kufuatia ongezeko la majeruhi na vifo kutoka machimboni, huku watoto wakiwa hatarini zaidi. Machimbo hayo ya mawe aghlabu hutumika kwa masuala ya ujenzi. Wakazi wa eneo hilo mara nyingi huchimba mchanga, na makampuni makubwa hukusanya saruji. Mwandishi Wetu Ferdinand Omondi alitembelea baadhi ya familia zilizoathirika kufahamu zaidi.