Tamasha la kimataifa la filamu lakamilika Zanzibar
Huwezi kusikiliza tena

Tamasha la filamu lakamilika Zanzibar

Tamasha kubwa la kimataifa, Zanzibar International Film Festival (ZIFF) limemalizika jana visiwani Zanzibar, ambalo mwaka huu limefanyika mara ya 18 tangu kuanzishwa kwake. Limepokea filamu zaidi ya 400 kwa mwaka huu pekee huku ukanda wa Afrika Mashiriki ukionyesha ushiriki mkubwa. Mwandishi wa BBC Sammy Awami alihudhuria siku ya mwisho ya tamasha hilo.