Mwili wa mgonjwa wa Ebola ukiondolewa eneo la tukio
Huwezi kusikiliza tena

Nyarugusu-Tanzania yahofia Ebola

Mtu mmoja kati ya wakimbizi kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Kaskazini Magharibi mwa Tanzania,amefariki dunia kutokana na ugonjwa unaodhaniwa kuwa ni Ebola.

Tayari uchuguzi wa kitabibu umeanza ili kuthibitisha kama mgonjwa huyo aliugua ebola au ni ugonjwa mwingine.

Hata hivyo madaktari mkoani humo wameshindwa kukanusha ama kuthibitisha juu ya kisa hicho kuwa ni ugonjwa wa Ebola hadi hapo matokeo ya uchunguzi huo yatakapokamilika.

BBC imezungumza na kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma huko nchini Tanzania Dr. Shija Ganai kujua undani wa kisa hicho.