Edward Lowassa
Huwezi kusikiliza tena

Lowassa achukua fomu za kuwania urais

Pilika pilika za uchaguzi nchini Tanzania zimeendelea huku Edward Lowassa, ambaye ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Chadema na kuungwa mkono na umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, UKAWA, akifika ofisi ya Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu ya urais. Lowassa alianadamana na mgombea mwenza Juma Duni Haji pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka vyama mbali mbali vya upinzani. Mwandishi wa BBC Sammy Awami alikuwepo eneo la tukio