Je hali ya wachimba dhahabu TZ itaimarika ?
Huwezi kusikiliza tena

Je hali ya wachimba dhahabu TZ itaimarika ?

Kwa watu wengi, pete ya dhahabu ni ishara ya upendo wa milele, lakini mara nyingine simulizi nyuma ya dhahabu hiyo huwa si ya kufurahisha sana.

Tanzania ni mzalishaji wanne wa dhahabu barani Afrika – lakini mamia ya maelfu ya wachimbaji wadogo wadogo nchini humo hufanya kazi katika mazingira magumu sana huku wakipata ujira mdogo na hata kuwa na matumaini madogo ya mafanikio yao.

Lakini inawezekana hili likabadilika kufuatia mpango mpya ulioandaliwa na shirika la Fairtrade kuuza dhahabu hiyo Uingereza – mpango huu ni wa kwanza wa aina yake barani Afrika.

Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anaarifu kutoka eneo la machimbo ya dhahabu nchini Tanzania