Huwezi kusikiliza tena

Watoto Albino wapatiwa viungo marekani

Watoto watano wa Tanzania wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya miili yao wamewekewa mikono na miguu ya bandia katika hospitali iliyopo nchini marekani. Watoto hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za kishirikina.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami, alizungumza na ofisa kutoka shirika la Under the Same Sun Martin Haule na alianza kwa kumuuliza ni watoto wangapi ambao wamepatiwa matibabu hadi hivi sasa?