Kitabu cha mafunzi ya ngono miongoni mwa watoto chazinduliwa Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Kitabu cha mafunzo ya ngono kwa watoto UG

Kwa wazazi wengi, ni vigumu kuzungumza na watoto wao kuhusu suala la ngono, na zaidi huwa mzazi hajui hata aanzie wapi.

Na kwa hivyo kuzungumza kuhusu unyanyasaji wa kingono au jinsi ya kuutambua na kusema unapotokea huenda ni changamto kubwa.

Kitabu kipya cha watoto chenye michoro kwa jina 'The Bad Touch', huenda ndio usaidizi kuanzisha mazungumzo ya aina hiyo.

Kitabu hicho, kilichozinduliwa siku ya ijumaa mjini Kampala, ni tamthilia ambapo mama anawaeleza watoto wake wawili kujifunza kusema hapana wanapoguswa vibaya.

Lillian Butele Kelle ni muandishi wa kitabu hicho. Ameeleza BBC kuwa nia yake ya kuandika kitabu hicho.