Huwezi kusikiliza tena

Watanzania washukiwa ugaidi Kenya

Polisi nchini Tanzania inafanya mpango wa kuwasilliana na wenzao wa Kenya ili kujua hatima ya Watanzania waliokamatwa nchini humo.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya kuwepo kwa taarifa za watanzania wanane kukamatwa nchini Kenya wakielekea Somalia kujiunga na Al Shabaab

Na ili kujua iwapo upande wa Tanzania unafahamu kuhusu kukamatwa kwa watanzania hao, sikiliza mahojiano kati ya Halima Nyanza na Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamishna Paul Chagonja.