Wagesa na Nyanswi ni wanawake walioona nchini Tanzania katika jamii ya Wakuria
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake kwa wanawake waoana Tanzania

Katika mila,desturi na tamaduni za makabila mengi muundo wa familia hasa ndoa hutofautiana, wakati mwingi zikiwa zikisihirikisha mwanaume na mwanamke.Katika mkoa wa Mara, wilaya ya Tarime, kaskazini mwa Tanzania, tamaduni za kizamani zinahusisha wanawake kuwaoa wanawake wenzao. Mwandishi wa BBC ,Tulanana Bohea anatuarifu zaidi vile muundo wa familia mbadala wa Nyumba ntobhu umebadilika na kuwa wa kisasa zaidi.