Huwezi kusikiliza tena

Vijana Mombasa, Kenya

Zaidi ya vijana 100 kutoka Mombasa wanaodhaniwa kuhamia nchini Somalia kujiunga na kikundi cha Al Shabaab, hawajulikani walipo.

Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amesema kuwa wengi wa vijana waliowahi kukamatwa na Polisi kwa shutma ya kuhusiana na Al Shabaab hawaonekani tena mitaani.

Lakini baadhi ya wazazi wanahofia kuwa watoto wao hao wamezimwa na serikali kinyume na sheria.

Sikiliza ripoti ya Ferdinand Omondi anaarifu zaidi.