Huwezi kusikiliza tena

Wanawake wahamasishwa kuwania uongozi TZ

Wakati joto la kisiasa likipamba moto huko nchini Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo mwezi Oktoba mwaka huu, jitihada za makusudi zimeanza kufanywa na baadhi ya taasisi za kiraia ili kuwajengea uwezo kina mama wajitokeze kwa wingi na kuwania nafasi mbali mbali za kisiasa.

Miongoni mwa walionufaika na mpango huo ni wale watokao maeneo mbali mbali ya nchi ikiwemo kaskazini mwa Unguja huko Zanzibar, maeneo ambayo mwanamke nafasi yake ni ndogo katika uongozi kutokana na mila na tamaduni. Mwandishi wetu Aboubakar Famau ambaye hivi karibuni alikuwepo mjini Unguja.