Huwezi kusikiliza tena

Filamu kumhusu Dokta Mukwege yazuiwa DRC

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo imepiga marufuku filamu inayomhusu Daktari wa upasuaji nchini humo Denis Mukwege ambaye aliwatibu maelfu ya wanawake waliobakwa wakati wa mapigano nchini humo.

Filamu hiyo kwa jina "The Man Who Mends Women," inaonyesha juhudi zake kujaribu kuwatibu majeraha wanawake waliobakwa na kudhalilishwa na wanajeshi wa nchi na pia waasi.

Akitoa tangazo hilo waziri wa habari Lambert Mende alisema filamu hiyo ina kusudia kuharibu sifa ya jeshi la nchi hiyo. Kufahamu zaidi sababu zilizosababisha filamu hiyo kupigwa marufuku Mwandishi wa Habari wa BBC, Lizzy Masinga alizungumza na mwandishi wa habari mashariki mwa Congo Byobe Malenga.