Mzazi akimbeba mwanawe mjini Alepo Syria
Huwezi kusikiliza tena

Mtoto aliyefariki baharini kuzikwa leo

Mvulana mchanga ambaye alizama baharini na kuifanya jamii ya Kimataifa kuimarisha juhudi zao za kutatua mzozo unaokumba Syria, atazikwa leo nyumbani kwao.

Baba wa mtoto huyo Aylan Kurdi aliruhusiwa kuingia mji wa Kobane kutoka Uturuki akiwa na jeneza la kubebea mwili wa mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu.

Mama wa mvulana huyo na kakake pia watazikwa hii leo.

Picha ya mwili wa mtoto huyo, ilisukumwa na mawimbi hadi ufuoni mwa bahari nchini Uturuki, hali iliyozua hamasa nyingi miongoni mwa jamii ya kimataifa kuhusiana na hatma ya watu wanaokimbia mapigano nchini Syria na kujaribu kuingia Ulaya.

Wakatu huo huo mgogoro umeonekana kushamiri kati ya polisi na maelfu ya wahamiaji waliokuwa wamelundikana ndani ya Treni, ambalo lililazimishwa kusimama katika mji wa Bicske, takriban kilomita thelathini kaskazini magharibi mwa Budapest.

Wahamiaji hao walikuwa na matumaini kwamba, treni hilo lingewapeleka kutoka Budapest hadi mpaka wa Austria. Abubakar Famao ana maelezo zaidi.