vibonzo
Huwezi kusikiliza tena

Vibonzo vyatumiwa kupasa ujumbe

Wengi huviita vibonzo vya Kingo,ambavyo nyuma yake yuko James Gayo, msanii na mchoraji nguli mwenye kufikisha ujumbe kwa hadhira yake kwa njia ya mzaha lakini ujumbe umesheheni ndani yake.

Vibonzo vya 'kingo' vimejizolea umaarufu mkubwa kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.

Sasa vibonzo vya Kingo vimeanza kutanua mawanda yake katika ukanda wa Afrika na kwa sasa vibonzo hivyo havichapishwi Tanzania pekee bali hata katika nchi za Kenya, Uganda na Zambia, huku dhima kubwa ya mvumbuzi ni kuhakikisha vibonzo hivyo havifi bali vinaishi

Tulanana Bohela alifanya mazungumzo na msanii huyo James Gayo ambaye awali anamuweka bayana mwalimu na makuzi yake.