Wanafunzi darasani
Huwezi kusikiliza tena

Mgomo wa waalimu Kenya waendelea

Chama cha muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Kenya COTU kimetoa ilaani ya siku saba kwa serikali, kutekeleza agaizo la mahakama kuu ya rufaa, la kuwalipa waalimu nyongesa ya mishahara ya kati ya asilimia 50-60.

Katibu mkuu wa chama hicho Francis atwoli amesema serikali ni sharti itekeleze agizo hilo la sivyo wafanyakazi wote wa umma wataanza mgomo wa kitaifa kuanzia wiki ijayo.

Waalimu nchini humo hawajarejea shuleni tangu muhula huu uanze na wameapa kutorejea hadi watakapoliwa nyogeza hiyo.

Mmoja baada ya mwingine viongozi hao waliikashifu serikali kwa kuwatelekeza wafanyazi wake.

Mwenyekiti wa chama cha waalimu nchini Kenya, Muzo Nzwili amesema serikali inaonyesha mfano mbaya licha ya kuwa mahakama hiyo ndio iliyowaweka madarakani.

Kwa upande wake katibu wa chama hicho Wilson sossion amesema wao wataendeleza juhudi hizo za kutaka kulipwa pasipo uoga wowote.

Mwakilishi wa wahudumu wa afya ambao kwa sasa wamegoma katika majimbo kadhaa alisema kuwa wao pia hawataendelea na mgomo wao sawia na wafanyakazi wengine.