Kibonzo cha kingo kutoka Tanzania chavuka mipaka
Huwezi kusikiliza tena

Kingo avuka mipaka ya Afrika mashariki

Nchini Tanzania kuna mchoraji mahiri wa vibonzo maarufu Kingo. Kingo ni kibonzo cha kuchekesha, na chenye busara katika magazeti ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 30. Hivi sasa Kingo ameanza kuvuka mipaka hadi nchi jirani za Kenya, Uganda na Zambia. Mchapishaji wake ni James Gayo aliyemfahamisha mwandishi wetu Tulanana Bohela kuwa nia yake ni kuona kwamba vibonzo vinaendelea kudumu.