jovago
Huwezi kusikiliza tena

Je waogopa kufanya manunuzi kimitandao?

Kampuni ya huduma za manunuzi ya kimtandao Barani Afrika JOVAGO inayohudumia zaidi ya nchi 40 za Afrika,hatimaye imeanzisha huduma za manunuzi na hivyo kuwa nchi ya pili baada ya Kenya kwa kuanza kunufaika na kuitumia kupitia simu yake ya mkononi. JOVAGO mtandao ulioanzishwa mwaka 2013 hadi sasa una takribani Hoteli 25,000 ndani ya Bara la Afrika.

Pamoja na malengo ya JOVAGO kurahisisha huduma hiyo,lakini pia JOVAGO wanaamini kuwa watachangia katika ukuaji wa utalii nchini Tanzania kama ilivyo kwa hali nyingine.

Lilian Kisasa ni Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo ya JOVAGO,katika mahojiano na Mwandishi wa BBC Leonard Mubali anaeleza jinsi ambavyo wanawasaidia wasafiiri na watalii kuvifahamu vivutio vya utalii vya ndani na nje ya maeneo yao na namna ya kuandaa safari zao.