Wanawake Lodwar
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake Turkana waungana kujiwezesha

Wanawake katika jamii ya Turkana, Kenya huchukuliwa kuwa bidhaa na mara nyingi hupigwa na kudhalilishwa wa waume zao. Lakini hali hii sasa inachukua sura mpya kwani wameanza kuungana na kujiwezesha kiuchumi.

Mjini Lodwar, kina mama ambao walikuwa wamepitia mateso mbali mbali wameunda kikundi cha kujiwezesha na kubadili mwenendo huo wa mfumo dume.

Mwandishi wa BBC Robert Kiptoo alitembelea kikundi hicho na kuandaa taarifa hii.