Huwezi kusikiliza tena

Mauaji ya vikongwe yatakoma Tanzania?

Katika mfululizo wa makala maalum kuhusu uchaguzi wa Tanzania leo tunaangazia tatizo la mauaji ya vikongwe huko Shinyanga kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambayo bado yanaendelea kuwa tatizo kubwa la eneo hilo.

Wananchi na baadhi ya ndugu walioguswa na mauaji hayo wanataka wagombea watakaochaguliwa baada ya uchugazi mkuu October 25 wachukue hatua kukomesha matukio hayo. Mwandishi wetu John Solombi aliyepo Shinyanga ametembelea familia iliyowahi kuathirika na mauaji hayo ambapo kijana alimuua mama yake mzazi kwa imani hizo.