Ungemuuliza  nini hayati  Nyerere angelikuwa hai ?
Huwezi kusikiliza tena

Ungemuuliza nini hayati Nyerere angelikuwa hai ?

Watanzania kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakitumia kitambulisha mada #DearNyerere kumkumbuka mwanzilishi wa taifa hilo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Sikukuu ya Nyerere Dei huadhimishwa kila Oktoba 14 kukumbuka siku aliyofariki kiongozi huyo.

Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Watanzania wamekuwa wakitumia vitambulisha mada kadha kueleza hisia zao kuhusu maono aliyokuwa nayo Bw Nyerere wakati wa uhuru 1961 na hali ilivyo sasa.

Mwandishi wetu pia amezungumza na baadhi ya wakazi ambao wanasema mengi ya maono ya Mwalimu Nyerere hayajatimia.