Wapiga kura
Huwezi kusikiliza tena

Majina ya wafu yadaiwa kuwa kwenye sajili

Wakazi katika maeneo mengi Zanzibar wamekuwa wakifika vituo vya tume ya uchaguzi kuhakiki taarifa zao kuhakikisha majina na maelezo kuwahusu yamenakiliwa vyema.

Baadhi wamedai kuona majina ya watu waliofariki kwenye sajili. Lakini mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Salum Kassim Ali amesema hilo ni jambo la kawaida na kusema raia ndio wenye jukumu la kufahamisha tume wapiga kura wanapofariki dunia.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau, aliyetembelea kituo cha shule ya upili ya Haile Sellasie, Unguja anasimulia.