Phindile Sithole-Spong
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke anayetetea walio na virusi vya Ukimwi

Idhaa ya Kiswahili ya BBC inaanza mfululizo wa makala maalum kuhusu wanawake wa Afrika na hatua walizopiga pamoja na changamoto zinazowakabili.

Katika wiki kadhaa zijazo tutakuletea makala hizo za wanawake wanaohamasisha jamii. Phindile Sithole-Spong, ni mwanaharakati kutoka Afrika Kusini, anaishi na virusi vya ukimwi, na anapambana na tatizo la unyanyapaa.