Walemavu
Huwezi kusikiliza tena

Wanariadha walemavu Kenya wakwama

Timu ya Kenya ya wanariadha walemavu imeshindwa kusafiri hadi Doha kushiriki mbio za Ubingwa wa Riadha Duniani baada ya serikali kuondoa ufadhili wake dakika za mwisho.

Mkuu wa kamati ya olimpiki ya wanariadha walemavu Agnes Oluoch, ameambia BBC kwamba ni ajabu serikali haina pesa za walemavu lakini ilifadhili “wanariadha wa kawaida asilimia 100”.

Mashindano hayo ni moja ya njia za wanariadha kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Rio 2016.

Anasimulia BBC kuhusu masaibu yao.