Lowassa:Vyombo vya dola vinatusakama bila sababu
Huwezi kusikiliza tena

Matokeo yanavyotolewa na tume ya uchaguzi TZ

Tume ya uchaguzi Tanzania imeanza kutangaza matokeo rasmi ya urais katika majimbo mbalimbali. Hatua hiyo ilianza siku ya jumatatu jijini Dar es Salaam. Matokeo hayo yamekuwa yakitolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva. Wakati hayo yakiendelea mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa amesema chama chake kinasakamwa na vyombo vya dola bila sababu.