Uchaguzi2015:Matukio mbali mbali TZ

MATUKIO MBALIMBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA

Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi

Image caption Dira ya dunia

6.00pm:Matangazo ya Dira ya dunia moja kwa moja kuanzia saa 6.30 hadi 7.30 jioni

5.56pm:Sababu 8 za kufutiliwa mbali kwa Uchaguzi Zanzibar.

Hizi ndozo sababu nane zilizotolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kisiwani Zanzibar kuhusu kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wa eneo hilo.

1.Makamishna wa uchaguzi katika tume hiyo walipigana kutokana na tofauti zao

2.Makamishna walikuwa na upendeleo fulani.

3.Katika vituo vyengine,hususan kisiwani Pemba,ambacho ni miliki ya Zanzibar,kura zilizopigwa zilikuwa zaidi ya zilizosajiliwa.

Image caption CCM

4.Masanduku ya kupigia kura hayakupewa ulinzi wa kutosha na maajenti pamoja na maafisa wa uchaguzi.

5.Maajenti wa vyama walifukuzwa katika vituo kadhaa.

6.Vijana walivamia vituo vya kupigia kura wakiwa na lengo la kuzua ghasia.

7.Vyama vya kisiasa vimekuwa vikiingilia tume hiyo.

8.Kura ziliharibiwa hususan zile kutoka Pemba.

Image caption Maalim Seif Hamad wa Zanzibar

5.31pm:Mgombea wa urais kupitia chama rasmi cha upinzani Kisiwani Zanzibar ameiambia BBC kwamba amesitikitishwa na hatua ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi katika kisiwa hicho.

Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa anaamini kwamba hatua hiyo ni ya mwenyekiti wa tume hiyo na wala sio ya makamishna.

Image caption Januari Makamba

Amewataka wafuasi wake kudumisha utulivu.

4.00pm:Chama cha CCM kimesema kuwa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar hakuwezi Kuathiri uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Msemaji wa kampeni za Chama hicho Januari Makamba amesema kuwa tume hizo mbili zinasimamiwa na katiba tofauti mbali na kusimamia maeneo tofauti.

3.27pm:'Kufutwa kwa matokeo ya Zanzibar hakutaathiri uchaguzi wa Tanzania bara',hayo ni matamshi ya mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Tanzania Damian Lubavu ambaye amesema kuwa uchaguzi unaosimamiwa na tume ya uchaguzi wa Zanzibar ni tofauti na ule wa Tanzania bara.

Image caption Ukawa

Damian Lubuva amesema kuwa tume zote mbili za uchaguzi zinasimamiwa na katiba tofauti licha ya kuwepo kwa muungano kati ya eneo la bara na lile la kisiwani Zanzibar.

Matamshi yake yanajiri mda mchache tu baada ya Muungano wa upinzani UKAWA kutaka uchaguzi wa Tanzania kufutiliwa mbali kufuatia hatua iliochukuliwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar.

2.28pm:UKAWA wataka uchaguzi kurejelewa Tanzania

Muungano wa upinzani chini Tanzania UKAWA umesema kuwa baada ya tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar kufutiliwa mbali matokeo ya eneo hilo uchaguzi wote nchini Tanzania unafaa kufutiliwa mbali.

Image caption ZEC

1.28pm:Matokeo yafutiliwa mbali Zanzibar

Matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar yamefutiliwa mbali.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kisiwani humo Jecha Salum Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

Image caption Tume ya uchaguzi Zanzibar

Kulingana na mwanahabari wetu aliye eneo hilo Sammy Awamy mwenyekiti huyo alitangaza hatua hiyo kupitia chombo cha habari cha mamlaka ya eneo hilo ZBC.

Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi.

Image caption Lowassa

1.17pm:Lowassa apinga matokeo ya uchaguzi.

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward LOwassa amesema kuwa hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC.Amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.

1.00pm:Vijana wa chama cha CHADEMA waliokamatwa na maafisa wa polisi wamewachiliwa bila kuwekewa mashtaka yoyote.

Wanasema kuwa walisafrishwa katika vituo tofauti vya polisi lakini wakaachiliwa bila laptopu na kompyuta zao.

Image caption Ridhiwani Kikwete

12.30pm:Mwana wa rais Kikwete wa Tanzania, Ridhiwani Kikwete amekihifadhi kiti chake cha jimbo la Chalinze. Ridhiwani aliyegombea kupitia chama cha CCM alijipatia kura 52,700 huku mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha CHADEMA Thorongey Mathayo akipata kura 20,153.

12.00:Magufuli achukua uongozi

Image caption Magufuli baada ya kupiga kura

Mgombea wa urais katika chama cha CCM John Pombe Magufuli anaongoza kwa kura zilizo hesabiwa kufikia sasa dhidi ya mpinzani wake Edward Lowassa huku ikiwa karibia nusu ya matokeo ya majimbo yametolewa.Ikiwa matokeo ya majimbo 133 kati ya 264 yametolewa na tume ya uchaguzi NEC,Magufuli ana asilimia 56.51 ikilinganishwa na Lowassa mwenye asilimia 41.67.

Image caption Vyombo vya habari

11.00am:Mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA Edward Lowassa atarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari mda wowote kuanzia sasa

10.30am:Chama cha ACT Zanzibar

Chama cha Uzalendo cha ACT kisiwani Zanzibar kimeiandikia barua tume ya uchaguzi kisiwani humo ZEC kikiitaka kutoa matokjo ya uchaguzi kwa haraka.Chama hicho kupitia naibu wake Ali Makame kinasema kuwa kutotolewa kwa matokeo hayo kunaathiri huduma kwa wananchi.

Image caption Magazetini Tanzania

10.00am:Vichwa vya habari vinavyogonga magazetini nchini Tanzania.

9.30am:Chama cha CCM kinachoongozwa na mgombea wa urais John Magufuli kimeshinda majimbo yote ya ubunge katika eneo la Dodoma huku muungano wa Ukawa chini ya uongozi wa Edward Lowassa ukichukua viti vingi katika mji wa Dar es Salaam.

9.00am:NEC yatoa ufafanuzi kuhusu matokeo

Image caption Damian Lubuva

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya rais kutoka majimbo mbalimbali akisema kuwa tume hiyo inatoa matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo yote nchini..Ameongezea kwamba hakuna mgombea wala chama kinachopendelewa katika suala la kutangazwa kwa matokeo na kwamba mshindi atapatikana tu kupitia kura nyingi.

7.00am:Washerehekea Kinondoni

Image caption Vijana kinondoni

Kulikuwa na sherehe katika jimbo la Kinondoni nchini Tanzania baada ya chama cha CUF kushinda katika eneo hilo.

Vijana waliokuwa wakifurahia ushindi huo waliimba na kuzunguka na bajaji wakiusifu ushindi huo na chama chao.

Image caption Maafisa wa polisi tayari kukabiliana na ghasia kinondoni

Hatahivyo maafisa wa polisi katika eneo hilo walifika katika eneo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea.

6.00am:Hali ya wasiwasi yatanda Zanzibar

Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.

Vyombo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza kuwa mshindi.

Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi yake.

UMEAMKAJE?

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza matokeo ya majimbo takriban 100 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.

Tunafuatilia pia hali ilivyo Zanzibar baada ya mtafaruku jana kuhusu kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wakati mmoja maafisa wa usalama walizingira kituo kinachotumiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutangaza matokeo na hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka. Tume ya uchaguzi humo visiwani kufikia jana jioni ilikuwa imetoa matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo yote 54.

Kwa habari zaidi kuhusu uchaguzi bofya Uchaguzi: #Tanzania2015