Lowassa
Huwezi kusikiliza tena

Lowassa aitaka tume imtangaze kuwa mshindi Tanzania

Mgombea urais wa chama cha Chadema Edward Ngoyai Lowassa ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais akidai alishinda uchaguzi huo.

Tume hiyo tayari imemtangaza mgombea wa chama tawala CCM John Pombe Magufuli kuwa mshindi akipata asilimia 58.46 ya kura. Bw Lowassa amekuwa wa pili na asilimia 39.97.

Msikilize Bw Lowassa akiwahutubia wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa rasmi.