Nkaissery
Huwezi kusikiliza tena

Nkaissery azungumzia kukamatwa kwa mwanahabari

Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Meja jenerali mstaafu Joseph Nkaissery ametetea hatua ya maafisa wa usalama kumkamata mwanahabari wa gazeti la Daily Nation nchini humo kwa tuhuma za kuandika taarifa ambazo kwa mujibu wake hazikufaa kuchapishwa.

Taarifa hiyo ilihusu madai ya kutumiwa vibaya kwa jumla ya Sh3.8 bilioni katika wizara ya usalama wa ndani.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Anthony Irungu.