Prof Jay Mikumi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Prof Jay amepanga yapi Bunge linapofunguliwa?

Bunge la Tanzania linafunguliwa Novemba 17 baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita. Miongoni mwa wanasiasa watakaoelekea bungeni mjini Dodoma siku ya ufunguzi ni wasanii mashuhuri wa Bongo. Mmoja wao ni Joseph Haule al maarufu Prof Jay aliyechaguliwa kama mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro.

Kabla ya kujitosa katika siasa, tungo za Prof Jay anayeimba kwa mitindo ya hip hop zilisifika sana kutokana na mashairi yake yaliyowasuta viongozi waliotoa ahadi zisizoweza kutekelezeka.

Arnold Kayanda alingumza naye katika studio zetu za Dar es salaam na kutuandalia taarifa ifuatayo.