Umehakikishiwa usawa kiasi gani?

Kwa kutumia kikokotozi hiki cha BBC, unaweza kujua hali ya pengo la usawa wa jinsia nchini mwako, na pale ulipo ukijilinganisha na wengine

Andika jina la nchi yako katika kijisanduku cha kutafuta kujua taifa lako limo nambari gani kwa usawa wa jinsia. Takwimu hizi za usawa wa jinsia zimetolewa kwenye ripoti ya World Economic Forum (WEF) iliyoangazia mataifa ambayo wanawake wana nafasi nzuri ya kushiriki kikamilifu katika maisha ya kisiasa na kiuchumi na kujivunia kufikia huduma za elimu na afya kwa usawa.

Vyanzo

World Economic Forum, Taasisi ya Takwimu ya Unesco, OECD

Njia

Katika kuandaa orodha hii ya pengo la jinsia duniani, World Economic Forum hutathmini makundi mbalimbali ya takwimu mbalimbali kuhusiana na kushirikishwa katika uchumi na kupewa nafasi, kupata elimu, afya, uwezo wa kuishi na kuwezeshwa kisiasa.

Orodha hii hufanywa kwa kuhesabu pengo la jinsia katika kufikia rasilimali na fursa zilizopo katika kila taifa. Hii huwezesha orodha hii kulinganisha mataifa tajiri na maskini kwa usawa.

Ripoti ya mwaka huu ndiyo ya 10 kutayarishwa na World Economic Forum na inaangazia nchi 145.

Takwimu kuhusu pengo la jinsia katika ulipaji wa mishahara zimetoka kwa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD). Takwimu za kila nchi ni zile za karibuni zaidi zilizoweza kupatikana na ni za kati ya 2010 na 2013.

OECD huhesabu pengo la mishahara kwa jinsia kama tofauti iliyopo kati ya kiwango cha kati wanacholipwa wanaume na wanawake ukilinganishwa na kiwango cha kati wanacholipwa wanaume. Takwimu zilizotumiwa ni za watu walioajiriwa kazi kikamilifu.

Takwimu kuhusu watu waliofuzu kutoka vyuo vikuu ambao ni wanawake zimetoka kwa Taasisi ya Takwimu ya Unesco.