Haben
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke afaaye wasioweza kuona na kusikia

Haben Girma ni mwanafunzi wa kwanza asiyeweza kuona au kusikia, kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Harvard. Ana lengo kubwa katika maisha. Alizaliwa California baada ya mama yake kukimbia kutoka Eritrea miaka ya 80, na kwenda Marekani kama mkimbizi. Alifaidika kutokana na sheria ya mfumo wa elimu nchini Marekani inayowapa haki walemavu, jambo ambalo kaka yake ambaye pia haoni alinyimwa nchini kwao Eritrea. Sasa hivi ni mwanasheria anayejitahidi kuimarisha upatikanaji wa teknolojia kwa watu wasioweza kuona au kusikia.