Huwezi kusikiliza tena

Mwalimu anayewapa moyo wanafunzi maskini Kenya

Jacqueline Jumbe-Kahura amezindua mfumo wa kipekee unaoshirikisha mahusiano baina ya walimu na wanafunzi.

Mfumo huu ambao unatilia mkazo walimu kuwa na uhusiano wa kibinadamu na wanafunzi wao imesaidia kupunguza migongano na hivyo kuimarisha viwango vya elimu katika kitongoji kidogo cha Kilifi katika pwani ya Kenya.

Shirika lake lisilokuwa la kiserikali LIBA (Lifting the Barriers) linawashughulikia wanafunzi katika shule 400 kwa kuwapa muundo mbinu mwafaka kwa elimu ikiwemo madawati, sare za shule na hata visodo kwa ajili ya watoto wa kike.